Youth Poetry Contest:Winning Pieces. Special recognition- TUMPE LIKIZO

FlyerMaker_09032019_100055.png

NAME: ZACHEUS MUKABANE MANDU(SPOKEN WIRD ARTIST)
STAGE NAME:. ZACSPEARE MANJU
INSTITUTION:. MACHAKOS UNIVERSITY(4TH YEAR)
TUMPE LIKIZO by Zacspeare Manju

Hino sauti yasikika tega sikio usikie
wengi wanateta wakiulizia ni nani alimpikia
alikuwa kichwa na sasa akili hana amekua mkia
heri pundamilia
si alikua simbaa mvinyo akabungia
ukampandisha tempo alipoamka keshowe akawa tembo
ikamtoka nembo maisha yakaanza kwenda kombo
hadi kikamtoka kimombo…alijuana na marijuana ikamteka akili sasa ashakua mahabusu.

Alikuwa na mipango ya kufanya harusi ila akavamiwa na ugonjwa wa kiharusi dunia ikamlamba kwa kisukari tajiri yamkini akakiri mihadarati zimemsaliti kisiri huku akisitiri shubiri.

Hili dua analoomba ni dua na kwa kweli limeabiri ndege
si Mola amwambie tu litafika lini kwake alijibu
si hata afikirie tu ni yeye mwalimu wa ishara hilo dua ni bubu
ni mengi sana yanomsibu moyoni ameyameza ila hawezi kuyatema anataka tu kuyasema
ugomvi umekita kambi ndani ya nafsi yake
anapong’ang’ana apate suluhu kumbe Ni dhambi tu anayotenda
hii kesi Ni ngumu na mahakama ishaamua kumuhukumu
kama Mola hutajibu dua lake anakunywa sumu
hivo basi pia wewe usije kumutuhumu
kisa na asili ya haya yote ni huyu msaliti mihadarati

Tendo,,tenda nikutende tanda nikutande
na kama umekua kuku si utage basi huenda vifaranga vitawa na huruma
hata ukatae nitavuma…
Hili swali Ni gumu Sana nauliza Mungu atalia hadi lini angalau chozi lisitoke
mikono yake imekwama kwenye tama hasira isitoke
anashinda akila sima kwa matoke hata yanuke
anauliza ni lini atakula nyama azipige dawa za kulevya mateke
zilimfanya rafiki yake asepe ilhali bado zinaongea matope
na kama kifo ndilo jibu basi anajitoa uhai
Alionja sigara ikawa wembe ikamkata na sasa hana tembe amekuwa mzembe

Ni mara ngapi nitawaambia Simba hawezi kula nyasi
Eti wa mkakasi uzuri ndani kipande cha mti, huo ni uswahili tu
Mbona basi akaamini huo msemo hadi akaabiri basi kwenda kuitafuta patasi

Image may contain: 1 person, smiling, sitting and shoes

Published by Stephen Ogweno

a global health practitioner, NCD advocate and mHealth Innovator

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: