
FEDINE BORIGA
THE WRITERS PEN
NAIROBI, KENYA
STUDENT RONGO UNIVERSITY
fedineboriga2016@gmail.com
(Download NCDs 365 App by clicking on the link below https://play.google.com/store/apps/details?id=com.stowelink.mcure )
JANGA LA CORONA
Corona kitimiri, sote twapenda kusikia
Vipi kuisitiri, mawazo kujipunguzia
Virusi visivyo na adhiri, mara Kwa mara kufuatilia
Mola tuepushe, janga hili la corona
Vifo twasuhudia, wapendwa kutuacha
Waalisaji kutusaidia, pate yake kubwa picha
Ndani kujitia, zimwi hili kujificha
Mola tuepushe, janga hili la corona

Uchumi meanguka, viwanda kasalia mahame
Usafiri umetatizika, yote haya ya mitume
Mazingira yamebadilika, sasa tujitume
Mola tuepushe, janga hili la corona
Watoto husika, wamechawa uchaji
Mimba za mapema kutendeka, hili kwao ni uborongaji
Majukumu kujitwika, masomo yaona utengaji
Mola tuepushe, janga hili la corona
Ndoa zimejaa doa, vyumbani kukaliki
Kazi kupotea, kila sekta ni taharuki
Wapi kujifichia, corona hapa haibanduki
Mola tuepushe, janga hili la corona

It was awesome working with you guys in creating awareness of metal effects of COVID 19
LikeLike